HabariMilele FmSwahili

Sharon Otieno kuzikwa leo Homabay

Sharon Otieno mwanafunzi wa chuo cha Rongo aliyeuwawa kinyama atazikwa leo kijiji cha Magare huko Homabay.Ni mazishi ambayo yatahudhuriwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa kutoka eneo hilo shinikizo zaidi zikitarajiwa kuelekezwa kwa serikali kuhakikisha haki inatendewa familia ya mwendazake.Mazishi ya Sharon yanawadia wakati washukiwa wakuu wa mauaji yake gavana Okoth Obado wa Migori, msaidizi wake Michael Oyamo na karani wa kaunti Caspel Obiero wakisubiri kubaini hatma yao tarehe 24 mwezi huu iwapo wataachiliwa kwa dhamana au la.

Show More

Related Articles