HabariSwahili

 Huzuni huku mwili wa Sharon Otieno ukipelekwa nyumbani kwa mazishi kesho 

Mwili wa mwendazake Sharon Otieno, aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo kaunti ya Migori, hatimaye umetolewa katika hifadhi ya maiti ya Kirindo na kuwasilishwa nyumbani kwao Magare kaunti ya Homabay, kusubiri mazishi hapo kesho.

Mwili huo umekuwa katika hifadhi hiyo kwa zaidi ya wiki  sita, huku uchunguzi ukiendelea kubaini waliotekeleza mauaji ya mwanafunzi huyo na kijusi cha miezi 7 tumboni mwake.

Mamake Sharon alizirai baada ya kulemewa na majonzi wakati mwili wake ulipowasilishwa  nyumbani Homa Bay.

Show More

Related Articles