HabariMilele FmSwahili

Matayarisho ya sherehe za Mashujaa Kakamega yakamilika

Maandalizi yamekamilika kwa ajili ya maadhimisho ya siku kuu ya Mashujaa katika kaunti ya Kakamega. Idara ya usalama inasema imeweka mikakati kabambe tayari kuwapokea zaidi ya watu elfu 60 watakaohudhuria hafla hiyo katika uwanja wa  Bukhungu. Rais Uhuru Kenyatta atarajiwa kuongoza hafla hiyo inayoandaliwa kwa mara ya kwanza katika eneo la Magharibi.

Show More

Related Articles