HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta ashauriwa kuongoza mikakati ya kumaliza vita vya ukoo Marsabit

Gavana wa Marsabit Ali Mohammed anamtaka rais Uhuru Kenyatta na waziri wa usalama wa kitiafa Dkt Fred Matiangi kuingilia kati mapigano baina ya jamii mbili yaliyochangia vifo vya watu 14 katika kaunti yake. Mohammed sasa anamtaka waziri Dkt Matiangi kuitisha mkao wa dharura utakaoangazia mgogoro huo ulioanza mwezi Septemba. Kadhalika ametaka suala la mpaka ambalo limetajwa kuchangia mapigano hayo kutatuliwa kwa njia ya uwazi.Gavana Mohammed kadhalika anadai maafisa wa usalama eneo hilo wamefeli kuwakamata wahusika licha ya kuwatambua vyema.

Show More

Related Articles