HabariPilipili FmPilipili FM News

Kongamano La SKAL Kuimarisha Utalii Asema Hersi.

Huku kongamano la kitalii la SKAL likiendele kaunti ya Mombasa mwenyekiti wa  shirikisho la utalii nchini Mohamed Hersi amesema kongamano hilo limeiletea kenya sifa na anauhakika sekta ya utalii itazidi kufunguka.

Akiongea katika kongamano hilo Hersi amesema  zaidi ya wageni 350 ambao wamekuja kwa kongamano hilo ni ishara ya ukuaji wa utalii nchini.

Wakati huo huo Hersi amedokeza kuwa kwa kipindi cha mwezi huu hadi Disemba kunatarajiwa watalii zaidi kutoka nchi za Uholanzi,Uingereza na marekani kuzuru taifa la kenya.

 

Show More

Related Articles