HabariPilipili FmPilipili FM News

Wario Na Keino Wamejiwasilisha Kwa Idara Ya Upelelezi.

Hatimaye aliyekuwa waziri wa michezo Hassan Wario na mwariadha mkongwe Kipchoge Keino wamejiwasilisha kwa maafisa wa polisi mapema leo kama walivyoagizwa na mahakama ya nairobi.

Wario na Keino wamekuwa nje ya nchi  kufikia usiku wa jumatano hapo jana .

Inaarifiwa wawili hao wamejiwasilisha kwa idara ya upelelezi wa jinai mapema leo asubuhi wakiandamana na mawakili wao kulingana na polisi.

Wengine waliojiwasilisha kwa polisi ni Haron Komen na Patrick Nkabu ambao pia ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakisakwa kuhusiana na ufujaji wa shilingi milioni 55 wakati wa mandalizi ya michezo ya olimpiki.

Show More

Related Articles