HabariMilele FmSwahili

Hassan Wario ajisalimisha kwa maafisa wa polisi alivyoagizwa na mahakama

Balozi wa Kenya nchini Austria Hassan Wario amejisalimisha kwa maafisa wa polisi kama alivyoagizwa na mahakama. Wengine wanaoarifiwa kujiwasilisha katika idara ya jinai saa 11 alfajiri ya leo ni Harun Komen, Patrick Kimithi na aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya olimpiki Kipchoge Keino. Wanne hao walikuwa wamepewa matakaa ya hadi leo kujiwasilisha kwa DCI la sivyo wakamatwe kwa kuhusishwa na sakata ya kupotea shilingi milioni 55 zilizotengewa kikosi cha Kenya kilichoshiriki mbio za olimpiki za Rio nchini Brazil mwaka 2016. Hakimu Mkuu Douglas Ogoti jumatatu wiki hii pia aliagiza kuwa wote wafikishwe mbele yake kesho saa mbili unusu asubuhi kujibu mashtaka. Wario ambaye alikuwa waziri wa michezo anatarajiwa kufunguliwa mashtaka 6 ya utumizi mbaya wa afisi.

Show More

Related Articles