HabariSwahili

Wanafunzi na walimu waanza kuona matunda ya mtaala uliozinduliwa

Mapema mwaka huu wizara ya elimu ilizindua mtaala mpya wa 2-6-6-3, mtaala unaosisitiza utendakazi katika madarasa matatu ya kwanza.
Haya yote licha ya kuwepo kwa upinzani kutoka baadhi ya wadau katika sekta ya elimu.
Na sasa kwa karibu mwaka mmoja tangu kung’oa nanga, walimu na wanafunzi wamesalia kuvuna matunda yake,haswa kutokana na jinsi wanafunzi wanavyopokea mafunzo kama vile maadili mema katika jamii.
Mwahabari wetu Shukri Wachu alitembelea shule ya msingi ya Nairobi na kutuandalia taarifa ifuatayo.

Show More

Related Articles