HabariMilele FmSwahili

Margaret Kenyatta:Kumekuwa na ufanisi katika kampeini ya kupunguza maafa ya akina mama wakijifungua

Mkewe rais Bi Margret Kenyatta anasema kumekuwa na ufanisi mkubwa katika kampeini ya kupunguza maafa yanayotokana na visa vya akina mama kujifungua.Na licha ya hatua ambazo amepiga kupitia kampeini yake ya Beyond Zero anasema ataendelea kushirikiana na kaunti mbalimbali kuwahimiza akina mama wajawazito kujifungua hospitalini.Alikuwa akizungumza kaunti ya Nakuru alikofungua rasmi kitengo cha kisasa cha kujifungua akina mama, kilichopewa jina lake, hospitali ya Nakuru Level 5.

Show More

Related Articles