HabariPilipili FmPilipili FM News

Mahakama Kuamua Kama Kesi Ya Naibu Jaji Mkuu Itaskizwa Na Majaji Watatu.

Mahakama kuu leo itaamua iwapo kuna ulazima wa kuunda benchi la majaji watatu kusikiza kesi ya ufisadi inayo mkabili naibu jaji mkuu Philomena Mwilu.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na jaji wa mahakama hiyo Chacha Mwita , ambaye hapo awali alitoa agizo la kuzuia kesi hiyo kuendelea kusikizwa.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajjji amekuwa akitaka faili ya mashtaka ya Mwilu, iwasilishwe kwa jaji mkuu David Maraga ambaye ana uwezo wa kuteua majaji watatu kusikiza kesi hiyo.

Aidha Hajji alipendekeza hatua hiyo kutokana na uzito wa kikatiba unaoizingira kesi hiyo.

Show More

Related Articles