HabariMilele FmSwahili

Mithika Linturi aunga mkono pendekezo la marekebisho ya katiba

Seneta wa Meru Mithika Linturi ameunga mkono pendekezo la kura ya maoni kuhusu  marekebisho ya katiba akisema litanufaisha taifa kwa ujumla. Akizungumza katika kaunti ya Meru Mithika amesisitiza kuhusu haja ya kupunguzwa nyadhifa serikalini ikiwemo idadi ya wabunge ili kumpunguzia mwananchi mzigo wa gharama ya maisha.Seneta huyo pia ameridhia mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa wabunge wanateuliwa kuhudumu kama mawaziri serikalini.

Show More

Related Articles