HabariPilipili FmPilipili FM News

Fedha Zakuandaa Kura Ya Maoni Zafaa Kufanyiwa Miradi Asema Mwadime.

Wito umetolewa kwa Serikali kutumia fedha wanazopania kuzitumia kwa kura ya maamuzi,  kutafuta wawekezaji ili kuwasaidia Wakenya kupata ajira sehemu mbali mbali nchini.

Hii ni kauli ya mbunge wa Mwatate  Andrew Mwadime ambaye anahisi ingekuwa vyema fedha hizo zitumiwe kuanzisha viwanda ili kubuni nafasi za kazi kwa wanchi mashinani.

Anasema iwapo kura hiyo ya maamuzi itaafikiwa huenda kukakosekana uwakilishaji unaohitajika hasa kwa jamii zenye idadi chache ya watu.

Show More

Related Articles