HabariMilele FmSwahili

Mahakama kuamua jumatano ijayo iwapo itawaachilia kwa dhamana Maribe na Irungu

Mahakama kuu itaamua jumatano ijayo iwapo itawaachilia kwa dhamana mwanahabari Jacque Maribe na mpenzie Joseph Irungu. Agizo hilo limetolewa na jaji wa mahakama kuu James Wakiaga ambaye ameagiza kikao cha kusikiliza ombi hilo kuandaliwa saa tano asubuhi siku hiyo. Wawili hao ambao wamepinga kuhusika katika mauji ya Monica Kimani mwezi uliopita wanataka kuachiliwa kwa dhamana huku kesi hiyo ikiendelea.Upande wa mashtaka hata hivyo umepinga kuachiliwa kwao ukidai huenda wakawatishia baadhi ya mashahidi.

Show More

Related Articles