HabariSwahili

Maurice Buluma aondolewa na wawakilishi kwa tuhuma za ufisadi 

Wawakilishi wadi wa bunge la Kakamega  wamemfurusha spika wa bunge hilo Maurice Buluma na kumteua Kennedy Kilwake.
Wawakilishi hao ambao wametekeleza uharibifu kwenye afisi za spika  huyo, wanadai anafaa kuondoka wakimtuhumu buluma kwa ubadhirifu wa fedha na kuwanyima wawakilishi mikopo ya kununua nyumba.
Wakati huo huo spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi ameongoza kamati ya mamlaka ya bunge kutembelea vyoo vya wabunge wa kike kutathmini uwezekano wa kusikika yaliyojiri wakati wa ripoti ya sukari.

Show More

Related Articles