HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Pwani Wahimizwa Kuhubiri Umoja.

Wakaazi wa ukanda wa pwani wamehimizwa kuungana ili kuhakikisha wanapata nafasi katika serikali kuu.

Akiongea wakati wakuchangisha fedha  za kuendeleza kanisa eneo la Kasemeni eneo bunge la Kilifi Kusini mbunge wa Ganza Teddy Mwambire amedokeza kwa muda mrefu kumekua na mgawanyika baina ya viongozi na wananchi katika eneo hili hivyo akasistiza uwepo wa umoja ili kutekeleza maendeleo ya kijamii na kisiasa.

Kauli ya Mwambire imeungwa mkono na mbunge wa Kilifi kusini Ken Chonga ambaye amewataka viongozi kuja pamoja kuwafanyia maendelea wakaazi wa pwani, huku akisema wakati wakuifanyia marekebisho katiba umefika  akiwataka viongozi wa dini kutoa mwelekeo mwafaka katika swala hilo.

Viongozi wengine waliohudhuria hafla hio ni mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi, Mishi Mboko wa Likoni, na mbunge wa Kaloleni Paul Katana.

 

Show More

Related Articles