HabariMilele FmSwahili

Raia wa Chad ashtakiwa kwa kumtapeli aliyekuwa mbunge Danson Mungatana

Raia wa Chad Abdoulayi Tamba amefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kumtapeli  aliyekuwa mbunge wa Garsen Danson Mungatana. Tamba anakabiliwa na shtaka kumlaghai Mungatana shilingi milioni 76 pamoja na kosa la kupatikana na  shilingi milioni 960 pesa bandia.Mshukiwa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3.Haya yanajiri huku Mungatana akitishia kulishtaki gazeti moja nchini kwa kumchafulia jina kuhusiana na sakata ya kutapeliwa.

Show More

Related Articles