HabariMilele FmSwahili

Manaibu kamishna na machifu kupokezwa mafunzo ya kijeshi katika miezi 6 ijayo

Zaidi ya manaibu kamishna 440 wa kaunti na machifu 3,400 watapokezwa baadhi ya mafunzo ya kijeshi katika muda miezi 6 ijayo. Waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiang’i anasema mafunzo hayo yatakayotolewa na idara ya polisi yanalenga kuboresha utendakazi wao. akizungumza huko Nnyeri mapema leo alipokutana na wakuu wa usalama, Matiang’i anasema hatua hii itahakiksiha maafisa hao wa umma wanatoa huduma bora za ulinzi.Matiang’i aidha amefichua uchunguzi unaendelea dhidi ya maafisa wa usalama wanaohudumu katika kaunti 2 wanaodaiwa kuchangia sakata ya uagizaji mahindi.

Show More

Related Articles