HabariPilipili FmPilipili FM News

Sonko Ahimizwa Kumteua Mwanamke Kama Naibu Wake.

Kinamama wameandamana jijini Nairobi mapema leo kumshinikiza gavana wa kaunti hiyo Mike Sonko kumchagua mama mwenzao kuwa naibu wa gavana.

Kina mama hao wanasema huduma muhimu zimeendelea kukwama jijini humo, kutokana na kutoteuliwa kwa naibu gavana kushirikiana na Sonko ili kuwahudumia wenyeji.

Wakati huo huo Kinamama hao pia wamewasilisha rasmi lalama zao kwa  afisi ya rais na naibu wake pamoja na ile ya  gavana Mike  Sonko.

Show More

Related Articles