HabariPilipili FmPilipili FM News

Wageni Wahakikishiwa Usalama Wao Mombasa Wakati Wa Kongamano La SKAL.

Idara ya usalama kaunti ya Mombasa imetoa hakikisho la kiusalama kwa zaidi ya wageni 500  wanaohudhuria kongamano la kimataifa la SKAL international, linalo tazamiwa kung’oa nanga rasmi hapo kesho.

Johnstone Ipara ambaye ni Kamanda wa polisi hapa mombasa anasema wameweka mikakati kabambe kuthibiti hali zote zinazoweza kutatiza  usalama kwa wageni hao na hata wenyeji.

Amewarai wananchi kushirikiana na maafisa wa polisi , hasa kwa kutoa taarifa pale wanapotambua wahalifu .

Kauli sawia imetolewa na kamishna wa kaunti ya mombasa EvansAchoki .

Show More

Related Articles