HabariMilele FmSwahili

Wauguzi Kenyatta wagoma wakilalamikia kujeruhiwa vibaya 1 wao

Wauguzi katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta wamesusia kazi leo kulalamikia ukosefu wa usalama wao hospitalini humo. Chini ya muungano wao, wauguzi hao wamesikitikia kisa ambapo mwenzao alivamiwa wikendi iliyopita na jamaa za mgonjwa aliyefariki hospitalini humo. Katibu mkuu Maurice Opetu ameelekeza kidole cha lawama kwa uongozi wa KNH kwa kutoweka mikakati ya kuwalinda wauguzi wanapotoa huduma zao Opetu ameitaka KNH kutoa matibabu ya dharura kwa mwenzao ambaye amelazwa kutokana na majeraha aliyopata lau sivyo wataichukua hatua za kisheria KNH

Show More

Related Articles