HabariMilele FmSwahili

Serikali yawahakikishia watahiniwa wote mazingira shwari ya kufanya mitihani yao

Serikali imewahakikishia watahiniwa wote wa mitihani ya kitaifa mwaka huu mazingira shwari ya kufanya mitihani yao. Waziri wa usalama wa kitaifa Dkt Fred Matiang’i amesema hakuna mwanafunzi atakayehamishiwa eneo jirani kutokana na sababu za kiusalama huku akitaja maeneo yanakokumbwa na changamoto za kiusalama yakimwemo kaunti ya Mandera kuwa miongoni mwa kutakakoshuhudia ulinzi mkali. Dkt Matiang’i pia ametangaza kuwa hakuna afisa wa polisi atakayeruhusiwa kwenda mapumziko msimu wa mtihani kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 29 mwaka huu. Ametoa onyo kali dhidi ya wanaonuuia kushiriki wizi wa mtihani kuwa watakabiliwa vikali kwa mujibu wa sheria.

Show More

Related Articles