HabariPilipili FmPilipili FM News

Maribe Na Jowie Wakanausha Mashtaka Ya Mauaji.

Mwanahabari Jacqe Maribe na mpenziwe Joseph Irungu wamekanusha mashtaka ya mauaji ya Monica Kimani yanayo wakabili.

Wawili hao  wamekana mashtaka hayo mbele ya jaji wa mahakama ya milimani  Jessie Lessit.

Maribe ataendelea kuzuiliwa rumande katika gereza la wanawake la Lang’ata, huku Mwenzake Joseph Irungu akizuiliwa katika gereza la Industrial Area, wakisubiri kurudishwa kotini siku ya jumatano.

Siku ya jumatano mahakama itaamua iwapo washukiwa hao wataachiliwa kwa dhamana au la, na pia kutangaza tarehe ya kusikizwa kwa kesi dhidi yao.

Show More

Related Articles