MichezoMilele FmSwahili

Harambee Stars yapokea zawadi ya shilingi milioni 3 kutoka kwa gavana Sonko

Timu ya taifa ya mchezo wa kandanda Harambee Stars imepokea zawadi ya dola elfu 30 sawa na shilingi milioni 3 kutoka kwa gavana wa Nairobi Mike Sonko. Gavana Sonko ametoa fedha hizo baada ya kuiahidi Harambee Stars kuizawaidia iwapo itaishinda timu ya taifa ya Ethiopia. Harambee Stars iliibuka mshindi kwa mabao 3 0 kwa mechi iliyochezwa jana.

Show More

Related Articles