HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta:Kenya haitaondoa wanajeshi nchini Somalia

Kenya haitaondoa wanajeshi nchini Somalia. Rais Uhuru Kenyatta anasema kuwa wanajeshi wa KDF walioingia nchini Somalia mwaka 2011 chini ya muungano wa Amisom watasalia nchini humo hadi mitandao yote ya kigaidi iliyo Somalia isambaratishwe. Akiongea wakati wa maadhimisho ya kuwakumbuka wanajeshi walioangamia wakiwa kazini huko Gilgil kaunti ya Nakuru, rais ametambua mchango wa wanajeshi hao na hatari inayowakumba  katika harakati za kulinda taifa. Rais anasema kuna haja ya mipaka ya Kenya kusalia salama jukumu ambalo linatekelezwa na wanajeshi wa KDF kwa uadilifu.

Show More

Related Articles