HabariMilele FmSwahili

Joseph Irungu na mpenzie Jackie Maribe wakanusha mashtaka ya mauaji

Joseph Irungu alaamurfu Jowie na mpenzie mwanahabari Jackie Maribe wamekanusha mashtaka ya mauaji. Wakiwa mbele ya jaji Jessi Lessit, wawili hao wamekana kuhusika wala kutekeleza mauaji ya Monica Kimani nyumbani kwake mtaani Kilimani hapa Nairobi mwezi jana.Jaji Lessit hata hivyo ameagiza pande husika katika kesi hii kufika mbele ya jaji mwengine jumatano ijayo ili kutoa muelekeo wa ombi la kuachiliwa kwa dhamana Jowie na Maribe.

Show More

Related Articles