K24 TvNEWSSwahiliVideos

UBOMOAJI WA JENGO LA SEEFAR: Yadaiwa jengo liko kwenye bwawa la Nairobi

Wawekezaji katika  nyumba za Seefar aparments , eneo la Highrise,  mjini Nairobi wanasema kuwa  halmashauri ya usimamizi wa maji nchini iliidhinisha ujenzi wa nyumba hizo na kwa hivyo hawaelewi ni kwa nini  halmashauri hiyo inataka kuzibomoa.

Wawekezaji hao pia wanapinga hatua ya halmshauri hiyo kuamuru wasimamizi wa  kampuni ya Edderman iliyojenga nyumba hizo kufika afisini mwake  hapo kesho, wakisema kuwa kampuni hiyo tayari imewauzia nyumba hizo, na hivyo wanastahili kujisimamia wenyewe.

Show More

Related Articles