HabariPilipili FmPilipili FM News

Basi Lateketea Kwa Njia Isiyoeleweka Katika Eneo la Samburu, Kwale.

Maafisa wa polisi eneo la samburu kaunti ya kwale wanachunguza kisa ambapo bus moja  ya kampuni ya modern coast  imeteketea moto kiasi cha kutotambulika  katika mazingira tatanishi  katika eneo hilo la samburu usiku wa kuamkia leo

Akithibitisha tukio hilo kamishna wa kwale  karuku ngumo amesema kuwa tukio hilo limetokea mwendo wa saa sita usiku wakati bus hilo lilipokuwa likielekea  mtito andei  kutoka mombasa  kwa masuala ya huduma za  dharura  .

Hata hivyo hakuna aliyejeruhiwa katika mkasa huo  kwani basi halikuwa limebeba abiria .

 

Show More

Related Articles