HabariPilipili FmPilipili FM News

Wabunge Wapendekeza Muda Wa Rais Kuhudumu Uwe Muhula Mmoja Miaka 7

Baadhi ya wabunge sasa wanapendeka sheria za wadhfa wa urais zifanyiwe mageuzi kuhakikisha rais anahudumu kwa muhula mmoja wa miaka 7 pekee.

Wabunge hao aidha wakiongozwa na mbunge wa Aldai Cornelius Serem wanapendekeza pia rais abadilishwe kutoka kwa jamii moja hadi nyingine, ili kila mwananchi ajihisi kuwakilishwa vyema uongozini hatua ambayo wabunge hao wanahisi itamaliza chuki za kisiasa na ukabila nchini.

Kuhusu pendekezo la idadi ya wabunge na wawakilishi wadi kupunguzwa ili kupunguza matumizi ya serikali na gharama kubwa kwa wananchi, wabunge wanahisi kuwa hilo linapaswa kujadiliwa baada ya watu kuhesabiwa mwaka wa 2019 ili ibainike maeneobunge yenye idadi ndogo ya watu.

Show More

Related Articles