HabariPilipili FmPilipili FM News

Wahudumu Wa tuk tuk Wadai Kunyanyaswa.

Wahudumu wa tuk tuk   katika kaunti ya Mombasa wamemtaka gavana Ali Hassan Joho kuingilia kati dhidi ya manyanyaso wanayopata kutoka kwa vyama vinavyo daiwa kusimamia sekta hiyo.

Wakiongea na wanahabari katika eneo la Changamwe wamedai kwamba wako zaidi ya wahudumu 7,000 na wanachangia pato la ushuru kwa kiasi kikubwa

Aidha wameongeza kuwa sekta hiyo imeanza kuwa na ubepari ambao huenda ukasambaratisha kabisa sekta hiyo.

Wamehoji kuwa vyama hivyo havijawahusisha washikadau hao kuhusiana  na mabadiliko hayo.

Show More

Related Articles