People Daily

Idadi Ya Watu Wanaopoteza Maisha Yao Kutokana Na Mauaji Ya Kiholela.

Visa vya ukosefu wa usalama mjini Mombasa vimetajwa  kuongezeka kwa miezi mitatu iliyopita huku idadi ya watu wanaopoteza maisha kutokana na mauji ya kiholela ikiendelea kushuhudiwa hali inayowafanya wakaazi kuishi kwa hofu na taharuki

Hii ni baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi tawi la Mombasa kuandamana kutetea haki ya mwanafunzi wa mwaka wa 4 Francis Odemba aliyekutana na mauti yake baada ya kuvumaniwa na umma kwa madai ya wizi usiku wa Jumanne eneo la KISAUNI.

Amos Kimanzi kiongozi wa wanafunzi kwenye chuo hicho  ametaka  haki kutendeka kwa mmoja wao na kutaka wananchi kususia kuchukua sheria mikononi na kuwaachia polisi kazi yao.

Naye afisaa wa kushughulikia masuala ya dharura katika shirika Muhuri Francis Auma amekashifu mauaji ya watu ambao hawana hatia akiwataka polisi kukomesha janga hilo mara moja kabla ya watu zaidi kupoteza maisha yao.

Show More

Related Articles