People Daily

Wazazi Wakiume Wadaiwa Kuchangia Kudorora Kwa Masomo Katika Eneo La Voi.

Wazazi wa kiume kaunti ya Taita Taveta hususan eneo bunge la Voi wamelaumiwa pakubwa kwa kuchangia kwa asilimia fulani kudorora kwa masomo ya watoto katika shule za msingi.

Haya yamesemwa na Mbunge wa eneo bunge la Voi Jones Mlolwa akisema wazazi wengi wa kiume wamewaachia wenzao wa kike jukumu la kuangalia familia huku wao wakijitokomeza kwa ubugiaji wa vileo.

Mlolwa ameeleza kusikitishwa na idadi kubwa ya wanaume kukosa kujihusisha na masomo ya watoto wao shuleni ikizingatiwa mikutano ya shule ikiitishwa wazazi wa kike ndio hupatikana bila kukosa.

Mbunge huyo amewaomba wanaume kubadilika na kuhusika kikamilifu katika agenda za maendeleo na kuwa mfano mwema katika jamii.

Show More

Related Articles