HabariMilele FmSwahili

Uchunguzi wa kiakili aliofanyiwa Maribe wabaini kuwa yuko katika hali sawa kiafya

Uchunguzi wa kiakili aliofanyiwa mtangazaji Jacque Maribe anayekabiliwa na kesi ya mauaji umebaini kuwa yuko katika hali sawa kiafya. Wakili wake Maribe Katwa Kigen amedhibitisha kuwa mteja wake anaweza kujibu mashtaka ya mauaji ya Monica Kimani. Maribe alifanyiwa uchunguzi huo kufuatia agizo la jaji wa mahakama kuu Jessie Lessit. Kesi dhidi yake inatarajiwa kuanza jumatatu juma lijalo.

Show More

Related Articles