HabariMilele FmSwahili

Mwanamume 1 amuua mpenziwe na kisha kujitia kitanzi Ainamoi

Huzuni imetanda katika kijiji cha Kiburet, eneo la Ainamoi baada ya mwanamume mmoja kumuua mpenziwe na kisha kujitia kitanzi usiku wa kuamkia leo.Mhusika mwenye umri wa miaka 25 anadaiwa kumdunga kisu mpenziwe wa miaka 22 kisha kuficha mwili wake mvunguni mwa kitanda.Chifu wa Ainamoi Richard Bett anasema wawili hao wamekuwa katika uhusiano huku akiongeza kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na kisa hicho.

Show More

Related Articles