HabariMilele FmSwahili

Obado kubaini hatma yake leo kuhusiana na kesi dhidi ya mauaji ya Sharon Otieno

Gavana wa Migori okoth Obado msaidizi wake Michael Oyamo na karani wa kaunti Caspel Obiero watabaini hatma yao leo kuhusiana na kesi dhidi yao ya mauaji ya Sharon Otieno. Jaji wa mahakama kuu Jessie Lessit atatoa uamuzi kwa ombi la watatu hao kuachiliwa kwa dhamana kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa. Jumatatu wiki hii jaji Lessit aliamuru kuzuiliwa kwao hadi leo kufuatia kujumuishwa kwa kesi zao. Tayari familia ya  Sharon Otieno imewasilisha ombi mahakamani kupinga kuachiliwa kwao ikidai huenda wakatatiza uchunguzi.

Show More

Related Articles