HabariSwahili

Mmiliki wa basi lililosababisha vifo vya watu 56 ashtakiwa

Mmiliki wa  basi lililosababisha  ajali iliyopelekea vifo vya watu  56 katika eneo la Kericho, na msimamizi wa chama cha ushirika  cha Western Cross Express SACCO wamezuiliwa na  mahakama ya Molo katika kituo cha polisi cha Londiani hadi hapo kesho,wakati uamuzi wa  ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana  utafanywa.
Hakimu mkuu Samuel Wahome , amewazuilia Bernard Ishindu na Cleophas  Shimanyula ili afanye uamuzi wa kina kuhusu ombi lao.
Haya yanajiri huku inspketa jenerali wa polisi Joseph Boinnet, akisema kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa maafisa wote wa polisi waliostahili kuwepo barabarani usiku wa mkasa .

Show More

Related Articles