HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Uhuru Atoa Wito Wa Ushirikiano Kwa Viongozi Hapa Nchini.

Rais Uhuru Kenyatta kwa mara nyingine amehimiza umoja na ushirikiano wa viongozi katika kutatua masuala yanayoathiri wananchi.

Akitolea mfano mzozo wa maji ambao umekuwepo kati ya viongozi wa kaunti ya Nairobi na ile ya Murang’a, rais Kenyatta amesema umoja wa viongozi ndio msingi wa kutatua mzozo kama huo, akiahidi ushirikiano wake katika mazungumzo ya kutafuta suluhu.

Aidha Rais Kenyatta amehimiza viongozi na wakenya kwa ujumla kuachana na siasa za mapema, na badala yake washirikiane kwa mambo muhimu ya kujenga taifa.

Show More

Related Articles