HabariPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa Wa Ugaidi Waachiliwa Huru Na Mahakama Ya Mombasa.

Wanawake watatu wanaokabiliwa na tuhuma za ugaidi wameachiliwa na mahakama ya mombasa hii leo kwa kukosekana ushahidi wa kutosha.

Watatu hao Ummulkheir Sadri Abdalla, Khadija Abubakar Abdulkarim na Halima Aden  walikamatwa mnamo machi 27 mwaka wa 2015 eneo la  Elwak , kwa madai walikuwa wanaelekea nchini Somalia kujiunga na kundi la kigaidi la alshabab.

Watatu hao aidha walifikishwa katika mahakama ya mombasa wakikabiliwa na mashtaka 20, ikiwemo kushirikiana na alshabab, kukusanya na kuzuilia taarifa kuhusu ugaidi , kupanga mafunzo ya kigaidi pamoja na mashtaka mengine.

Katika uamuzi wake wakati wa kuwaachilia watatu hao hakimu mkuu wa mahakama ya mombasa Evans Makori amesema upande wa mashtaka ulishindwa kuwasilisha ushahidi dhidi ya washukiwa.

Show More

Related Articles