HabariPilipili FmPilipili FM News

Wasichana Wa Dini Ya Kislamu Wadaiwa Kupotoka Kimaadili.

Asilimia 15 -20 ya wasichana wa dini ya kislamu Kaunti ya Mombasa wanadaiwa kupotoka kimaadili kufuatia mizozo baina ya wazazi wao ambayo imekuwa ikichangiwa na utumizi wa dawa za kulevya.

Asilimia hiyo imetajwa kuchangia ongezeko la uasherati na mimba za mapema miongoni mwa wasichana hao jambo linalotajwa kuongeza idadi ya kinamama wasiokuwa na waume, kinyume na maadili ya dini ya kislamu.

Sheikh Mohamed Khalifa ni Katibu mkuu wa Baraza la wahubiri na maiman nchini CIPK.

Khalifa aidha amewahimiza wazazi kuwajibika zaidi katika majukumu yao ya ulezi  na kuhakikisha wanakuwa mfano bora hasa kwa watoto wa kike kwa kuwaelekeza kuambatana na mafunzo ya dini hiyo

Show More

Related Articles