HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanamziki Joseph Kamaru Apumzishwa Nyumbani Kwake.

Rais Uhuru Kenyatta naibu wake William Ruto, pamoja na  kinara wa ODM Raila Odinga wameongoza mamia ya wakenya adhuhuri ya leo kwa mazishi ya mwanamziki Joseph Kamaru.

Akiongea wakati wa mazishi hayo kinara wa ODM Raila Odinga amemsifia marehemu kutokana na mchango wake mkuu kwa sanaa ya mziki humu nchini.

Aidha kuhusu ushirikiano wake na rais Uhuru Kenyatta Odinga amesema mwafaka wao hauhusiani na siasa za mwaka wa 2022 , akiwataka wakenya wote kuunga mkono mwafaka huo.

Kauli ya Raila imeungwa mkono na naibu rais William Ruto akisema wataendelea kushirikiana pamoja kama viongozi, ili kuunganisha wakenya na kufanikisha maendeleo.

Kamaru alifariki wiki iliyopita akipokea matibabu katika hospitali ya MP  Shah jijini Nairobi.

Show More

Related Articles