HabariMilele FmSwahili

Maduka mengi Nairobi yatii agizo la serikali kupunguza bei ya unga wa ugali

Maduka mengi ya jumla hapa Nairobi yametii agizo la serikali kupunguza unga wa ugali kwa shilingi 75 kwa kilo 2.Akiongoza oparesheni ya kufuatilia utekelezaji agizo hilo mkuu wa utoaji leseni Nairobi Michael Akoko anasema wameridhishwa na jinsi maduka mengi ya jumla yameanza kutekeleza agilo hilo lilitolewa na rais Uhuru Kenyatta mbali na waziri wa kilimo mwangi Kiunjuri.Hata hivyo mkuu wa kitengo cha utekelezaji kaunti ya Nairobi Tito Kilonzo anasema wanalenga kuangazia jinsi ya kukabili wale wanaokiuka agizo hilo.

Show More

Related Articles