HabariPilipili FmPilipili FM News

Mzoga Wa Papa Wapatikana Katika Fukwe Za Bahari.

Mzoga wa papa aina ya papa shilingi umepatikana katika fukwe ya bahari huko Diani kaunti ya Kwale.

Lilian Daudi afisa kutoka kitengo cha utafiti wa viumbe vya bahari KEMFRI anasema papa huyo alipatikana akiwa hali mahututi na kufa baada ya muda mchache  akiwa na uzito wa tani moja na nusu na urefu wa mita 3.6.

Peter Msembi afisaa wa kitengo hicho ameeleza kuwa kwa sasa wamechukua sampuli za papa huyo ili kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake.

Ikumbukwe kuwa ni hivi majuzi tu ambapo mzoga wa nyangumi ulipatika katika fukwe katika kaunti hiyo hiyo.

Show More

Related Articles