HabariMilele FmSwahili

Kassaine aliyekuwa akihojiwa kuhusiana na mauaji ya Monica aachiliwa huru

Mfanyabiashara Brian Kassaine aliyekuwa anahojiwa kuhusu mauaji ya Monica Kimani ameachiliwa huru.Jaji Joseph Kituku wa mahakama ya Kiambu amemuondolea lawama ya mauaji Kasaine ambaye amekuwa korokorioni kwa siku 13.Aidha Jaji Kituku amemtaka kasaine kupiga ripoti kila alhamisi katika makao makuu ya idara ya jinai DCI katika muda wa miezi miwili ijayo ili kusaidia katika uchunguzi. Akizungumza nje ya makao ya DCI Kasaine ameelezea furaha yake kwa kuachiliwa huru akipongeza idara ya uchunguzi kwa hatua hiyo .Kasaine anadaiwa kumiliki wa bastola iliyodaiwa ndio mshukiwa Jospeh Irungu aliitumia kujipiga risasi begani. Tayari upande wa mashtaka umedokeza nia ya kumtumia Kasaine kama mmoja wa mashahidi katika kesi hiyo.

Show More

Related Articles