HabariPilipili FmPilipili FM News

Mmiliki Wa Basi Lililosababisha Vifo Vya WATU 55 Atiwa Mbaroni.

Maafisa wa polisi wamemkamata mmiliki wa basi lililosababisha vifo vya watu 55 kaunti ya Kericho mapema jana.

Bernard Ishindu Shitiabayi mmiliki wa basi hilo la Home Boys na ambalo linaendeshwa na kampuni ya sacco ya Western Cross Express alikamatwa jana jioni huko Kakamega.

Kamanda wa polisi kaunti ya Kericho James Mogera anasema Shitiabayi alikamatwa pamoja na Cleophas Shimanyula ambaye ni mwanachama mkuu wa Sacco ya basi hilo.

Wawili hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kakamega.

Kulingana na ripoti basi hilo lilikuwa limebeba abiria kupita kiasi na lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi.

Show More

Related Articles