HabariMilele FmSwahili

Mmiliki wa basi lililohusika kwenye ajali Fort Ternan kufikishwa mahakamani leo

Mmiliki wa basi lililohusika kwenye ajali mbaya iliyosababisha vifo vya watu 56 katika bara bara eneo la Fort Ternan Kericho anafikishwa mahakamani leo. Bernard Shitiabai pamoja na wanachama kampuni ya Western Cross Cleophas inayomiliki basi hilo na Cleophas Shimanyula watashtakiwa katika mahakama ya Londiani kaunti ya Kericho. Inadaiwa basi hilo halikwua na kibali cha kuhudumu usiku, huku pia likidaiwa kuwabeba abiria kupitia kiasi. Joseph Chebii ni OCPD wa Kakamega.

Show More

Related Articles