HabariMilele FmSwahili

Asilimia 30 ya wagonjwa katika hospitali za Kisumu wanaugua ugonjwa wa akili

Imebainika asilimia 30 ya wagonjwa wanaotibiwa kwenye hospitali za kaunti ya Kisumu wanaugua ugonjwa wa akili.Waziri wa afya kaunti hiyo Rosemary Ombara amehusisha matumizi ya mihadarati na msongo wa mawazo kama sababu kuu ya kuwepo ugonjwa huo.Amesema serikali ya kaunti inalenga kuanzisha vituo vya kurekebisha tabia na kutoa uhamasisho kuzuia ongezeko la visa hivyo.

Show More

Related Articles