HabariMilele FmSwahili

Serikali ya kaunti ya Kericho kugharamia malipo ya hospitali kwa walionusurika kwenye ajali

Serikali ya kaunti ya Kericho itagharamia malipo ya hospitali kwa walionusurika kwenye ajali ya Fort Ternan na ambao wanauguza majeraha katika hospitali kadhaa kaunti hiyo.  Gavana Paul Chepkwony pia ametoa wito kwa wahisani kujitokeza kuchangisha damu kwa ajili ya manusura hao. Kadhalika miili ya watu 30 waliofariki kwenye ajali hiyo bado haijatambulika na jamaa zao kufikia sasa. Hayo yanajiri huku ikiarifiwa kuwa chumba cha maiti cha hospitali ya Kericho kinakabiliwa na msongamano wa miili ikizingatiwa kuwa kinaweza kuhifadhi miili 15 pekee.

Show More

Related Articles