HabariMilele FmSwahili

Serikali kuendelea na ubomoaji wa  majengo yaliyo kwenye ardhi ya umma kuanzia jumatatu

Serikali  itarejelea zoezi la ubomoaji wa  majengo yaliyo  kwenye ardhi  ya umma  na kwenye chemi chemi za maji kuanzia jumatatu juma lijalo.Ni   usemi wake katibu wa wizara ya ujenzi Prof Paul Maringa anayesema  majumba 12 yanalengwa kwenye oparesheni hiyo  ambayo ilikuwa imesitishwa kwa muda.Anasema wamiliki wa majengo hayo haramu na wahusika wa ujenzi huo wataandamwa ili kugharamia zoezi la ubomoaji.Amesema haya baada ya kuongoza shughuli ya kufungua sehemu  ya kupitisha  maji  kwenye mto ulio karibu na  jumba  lililobomolewa la Southend msimu wa mvua ukikaribia.

Show More

Related Articles