HabariPilipili FmPilipili FM News

Rais Kenyatta Aagiza Chanzo Cha Ajali Ya Kericho Kuchunguzwa.

Rais Uhuru Kenyatta katika ujumbe wake kupitia Twitter amezitaka idara husika kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakaopatikana na hatia.

Rais Kenyatta amewataadharisha madereva dhidi ya kuendesha magari kiholela.

Amesema waendesha magari wote wanapaswa kuwa waangalifu ili kuepusha ajali na vifo bara barani.

Naye insepekta generali wa Polisi Joseph Boinett amesema mmiliki wa SACCO ya basi hilo atashtakiwa kwa kuruhusu basi hilo kuendeshwa masaa ambayo hayaruhusiwi.

Kwa sasa maafisa wa polisi na mamlaka ya NTSA inawasaka wamiliki wa SACCO ya basi hilo.

Viongozi mbali mbali wametuma risala za rambi rambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

Show More

Related Articles