HabariMilele FmSwahili

Walimu 2 wauwawa na kundi la kigaidi la Al shabaab Mandera

Walimu wawili wameuwawa kufuatia shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab katika eneo la Mandera Mashariki. Washambuliaji waliojihami kwa risasi walifyatua risasi na kurusha kilipuzi katika makazi ya walimu katika shule ya upili ya wavulana ya Arabia. Wawili  hao ambao hawakuwa wenyeji  waliwauwa huku wengine wawili wakifanikiwa kutoroka. Aidha polisi wawili wa akiba waliokuwa wakilinda shule hiyo walilazimika kutoroka baada ya kuzidiwa nguvu na washambuliaji.

Show More

Related Articles