People Daily

Biashara ya majeneza yazua hofu Miongoni Mwa wananchi, Mombasa.

Baadhi ya wagonjwa wanaotafuta huduma za matibabu katika zahanati kuu ya makadara hapa mombasa wameeleza kuwa wao Hupatwa na hofu pale wanapoyaona majeneza yakiiuzwa kando kando ya hospitali hiyo.

Wakiongea na meza yetu ya habari baadhi ya wale  tulioweza kuzungumza nao wameiomba serikali kuwatengea mahali mbadala watengenezaji wa majeneza  ili kuondoa biashara hiyo karibu na hospitali

Kwa upande wao wauzaji  wameisifia biashara hiyo kutokana na faida kubwa wanayopata ,kwani  wao hupata wateja kila siku, huku  jeneza la bei ghali likiuzwa kwa zaidi ya shilingi elfu 100. Pia Wameeleza kuwepo changamoto za kijamii kuikosema maana  kazi hiyo, na baadhi ya watu kuwachukulia kama wenye nia mbaya.

Show More

Related Articles